Saturday, December 30, 2017

Christiano Ronaldo's story

WEMA HAUPOTEI.

Ilikuwa Jumamosi usiku 24 Mei 2014 pale Lisbon baada ya Madrid kuipiga Atletico 4-1 kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Christiano Ronaldo alionekana akivua jezi yake na kumpa mtu katika umati, ambaye alimwalika kuingia uwanjani na  kusherehekea pamoja naye...

Ilionekana ajabu kwa Ronaldo kusherehekea na shabiki wa kawaida sana! Wengi walioliona tuki hili walikimbilia mtandaoni kujaribu na kutafuta mtu huyu alikuwa nani...

Mtu huyo alijulikana kama Alberto Fantrau, jamaa ambaye alikulia mtaa mmoja na Ronaldo utotoni. Kukulia mtaa mmoja tu ndo kumesababisha urafiki wote huu!?!? Hapana...

Alipopokea tu tuzo zake hivi karibuni, Ronaldo alisema;
"Shukrani zimwendee Alberto Fantrau." Kisha akasema: "Naam, mimi ni mchezaji bora na mafanikio yangu yote yamesababishwa na rafiki yangu Alberto." Watu walitazamana na kuulizana, "Huyu Fantrau ni nani?" Kisha Ronaldo aliendelea kusema:

"Tulicheza pamoja katika timu ya vijana. Watu wa Sporting Lisbon walikuja kutazama. Walituambia kuwa mshambuliaji ambaye angefunga magoli mengi zaidi watamchukua.
Siku hiyo tulishinda 3-0. Nilifunga goli la kwanza, na kisha Albert alifunga la 2 kwa kichwa. Goli la 3 ndio lililovutia kila mtu. Alberto alianza kutokea kwa pembeni, kisha akajikuta uso kwa uso na kipa. Alimpunguza kipa na kujikuta yeye na goli tu, kiasi kwamba ilikuwa ausukume tu golini mpira. Wakati huo nilikuwa nakimbilia upande wake. Na badala ya kufunga, Alberto aliamua kunipasia mpira na mimi nikafunga. Hivi ndivyo nilivyojikuta katika Sporting Lisbon Academy."

"Baada ya mchezo nilimfuata, nikamwuliza. "kwa nini ulifanya vile?" Naye akajibu, "Kwa sababu najua kwamba wewe ni bora kuliko mimi."

Waandishi walipenda kujua zaidi. Walianza kuchunguza na kuweza kukutana na Alberto Fantrau kumwuliza kama hadithi waliyoambiwa na Ronaldo ni kweli. Alithibitisha, akiongeza kuwa kazi yake kama mchezaji wa mpira wa miguu ilimalizika baada ya mechi ile, wakati ilikuwa nafasi ya pekee kuwa mchezaji mahiri kama angeajiriwa na Sporting Lisbon. Badala yake amejikuta akibaki mtaani bila ajira.
Hata hivyo, waandishi wa habari, waliangalia nyumba yake ya kifahari na Mercedes benz anazomiliki wakamuuliza Alberto, "huna ajira yoyote, je ni jinsi gani unaweza kuwa na nyumba na gari za kifahari? Hauonekani kuwa na kipato cha kumiliki hivi vitu. Alberto alijibu, "Hiyo yote? Ni Ronaldo."

TUNAJIFUNZA NINI?
Hebu tujiulize swali lifuatalo: Je! Wangapi wetu tumefanya kitu kama Ronaldo na Alberto? Kwa kinyume chake, wengi wetu tunaonyesha kinyume cha hadithi hii inayoonyesha ubinafsi na msamaha kwa wenzi wao.
Marafiki! Hebu tusaidiane ili tuwe na fahari ya mafanikio ya ndugu / dada / marafiki / jamaa zetu.

No comments:

Post a Comment

Broken Things